Home Habari Kuu Rais Ruto: Sina tatizo na Raila kuandaa maandamano

Rais Ruto: Sina tatizo na Raila kuandaa maandamano

0

Rais William Ruto amesema hana shida na kinara wa upinzani Raila Odinga kuandaa maandamano.

Rais Ruto amesema maandamano ni nguzo moja ya kidemokrasia, jinsi ilivyoratibiwa kwenye katiba ya Kenya.

Akizungumza katika mahojiano na runinga ya France 24, Ruto alisema maandamano hayo hayafai kusababisha uharibifu wa mali na biashara za Wakenya walio na bidii.

“Sina shida na Raila Odinga kuandaa maandamano. Kile ambacho nimemweleza Odinga na washirika wake ni kwamba wasijihusishe katika uharibifu wa mali,” alisema Rais Ruto.

Matamshi yake yaliungwa mkono na katibu mkuu wa chama cha UDA Cleophas Malala, aliyehimiza Azimio kushiriki maandamano ya amani wanapotoa maoni yao kuhusu Mswada wa Fedha wa mwaka 2023.

“Tuna jukumu la kulinda taifa letu dhidi ya walioshindwa katika uchaguzi, na ambao hawachoki kusambaratisha uchumi wetu kila baada ya miaka mitano,” alisema Malala.

Muungano wa Azimio umesema utaandaa mkutano wa mashauriano siku Jumanne Juma lijalo, kujadili mswada huo ambao umepitishwa bungeni na unasubiri tu kutiwa saini na Rais Ruto ili kuwa sheria.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here