Home Habari Kuu Rais Ruto na Raila Odinga wakutana nchini Uganda

Rais Ruto na Raila Odinga wakutana nchini Uganda

0

Rais William Ruto na kiongozi wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga walifanya ziara nchini Uganda na kukutana na Rais Yoweri Museveni.

Rais Ruto aliashiria kuwa mkutano huo uliandaliwa kujadili maswala muhimu ya nchi hizo mbili kama vile nishati na mafuta.

Na wakati Raila tayari ameelezea nia ya kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, AUC, Rais Ruto aliashiria kuwa mkutano wao uliofanyika nyumbani kwake Museveni katika eneo la Kisozi, pia uliangazia azima ya Raila.

“Tulijadili azima ya Raila ya kuwania uenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika,” alisema Rais Ruto.

Kwa upande wake, Raila alisema mkutano huo ulijadili utangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, huku akiongeza kuwa azima yake ya kuwania uenyekiti wa AUC ilipewa kipaumbele.

Rais Museveni amesemekana kuunga mkono azima ya Raila.

Rais Ruto akutana na Raila nchini Uganda.

Raila alitoa shukran zake kwa Rais Ruto kwa kuunga mkono azima yake hiyo.

Punde tu baada ya Raila kutangaza kuwa atawania wadhifa huo, maafisa wa ngazi za juu katika serikali ya Rais Ruto, waliahidi kumuunga mkono na kuhakikisha anamrithi Moussa Faki ambaye muhula wake unakaribia kukamilika.

Kinyang’anyiro hicho kinaonekana kushika kasi huku Rais Ruto akiwa tayari amekutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed.

Mkutano kati yao ulifanyika katika Ikulu ya Nairobi siku ya Jumanne.

Website | + posts