Home Habari Kuu Rais Ruto: Mchango katika hazina ya NSSF kuongezeka hadi shilingi trilioni moja

Rais Ruto: Mchango katika hazina ya NSSF kuongezeka hadi shilingi trilioni moja

Kiongozi wa taifa alisema taifa hili limekumbatia mfumo wa uwekaji akiba, ili kubuni uwekezaji wa rasilimali wa muda mrefu.

0

Serikali inalenga kuongeza mchango katika hazina ya malipo ya uzeeni NSSF hadi shilingi trilioni moja kufikia mwaka 2027. Hayo yalisemwa na Rais William Ruto.

Kiongozi huyo wa taifa alisema taifa hili limekumbatia mfumo wa uwekaji akiba, ili kubuni uwekezaji wa rasilimali wa muda mrefu.

“Mfumo mpya wa hazina ya NSSF umeongeza mara nne mchango katika hazina hiyo. Mchango katika hazina hiyo utaongezeka kwa shilingi bilioni 400 katika muda wa miaka mitano ijayo…..na kufikia shilingi trilioni moja kufikia mwaka 2027,” alisema Rais Ruto.

Akihutubia taifa wakati wa sherehe ya Jamhuri katika bustani ya Uhuru Gardens Jijini Nairobi, Rais Ruto alidokeza kuwa wakenya sasa hawatasubiri muda wa miezi mitatu kupata marupurupu yao ya kustaafu, lakini sasa watapokea katika muda wa siku kumi.

“Wananchi sasa hawatasubiri miezi mitatu kupokea marupurupu yao ya kustaafu. kutokana na mfumo mpya, sasa watapokea fedha hizo ndani ya siku kumi,” alisema Rais Ruto.