Ziara ya Rais William Ruto katika eneo la Nyanza, itaingia siku pili Jumamosi akizuru kaunti ya Homabay.
Ruto atazindua ujenzi wa barabara ya kisiwa cha Mfangano eneo bunge la Suba Kaskazini.
Barabara hiyo inatarajiwa kuwekwa lami.
Ruto baadae atazuru shamba la kukuza samaki la Victory , eneo bunge la Suba Kusini na baadae azindue uwekaji lami wa barabara ya Sindo-Karungu-Mbita .
Pia Jumamosi mchana Ruto atafungua ufunguzi wa afisi ya chama cha United Democratic Alliance mjini Homa Bay na baadae kuzindua ukarabati wa kituo cha Bay Pier.
Ruto yuko ziarani eneo hilo la Luo Nyanza kwaziara ya siku nne ambapo kilele chake ataongoza mkutano wa baraza la mawaziri.