Rais William Ruto anatarajiwa kuondoka nchini Jumamosi usiku kwa ziara rasmi ya siku tatu nchini Uchina.
Ruto anatarajiwa kuhutubia kikao cha tatu cha mpango wa miundo msingi ya barabara cha Belt and road iniative BRI, ambacho kitaandaliwa mjini Beijing na kuhudhuriwa na viongozi kutoka mataifa mbali mbali.
Ruto atahutubia kikao hicho kuzungumzia kuhusu uchumi wa kidijitali maarufu kama Digital Economy as a new Source of growth.
Rais pia atafanya kikao na mwenyeji wake Rais Xi Jinping na viongozi wengine duniani kuhusu jinsi ya kushirikiana.
Kingozi wa taifa pia anatarajiwa kukutana na waekezaji wa Uchina katika meza ya mazungumzo kuangalia jinsi ya kushirikiana kuwekeza nchini Kenya.