Home Habari Kuu Rais Ruto kuzuru Bungoma Alhamisi

Rais Ruto kuzuru Bungoma Alhamisi

0

Rais William Ruto anatarajiwa kuanza ziara ya kuzindua miradi ya maendeleo katika kaunti ya Bungoma kuanzia Alhamisi Februari mosi.

Ziara hiyo inajiri miezi mitano tangu alipozuru kaunti ya Bungoma .

Ruto ataanza ziara katika shule ya Naitiri ambapo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa soko la Naitiri, kabla ya kuelekea Webuye West, atapoongoza utoaji malipo kwa wakulima waliowasilisha miwa kwa kampuni
ya sukari ya Nzoia.

Pia Rais ataongoza ugavi wa mbolea iliyopunguzwa bei kwa wakulima katika eneo hilo la Webuye West.

Ziara ya mwisho ya Rais itakuwa eneo la Bungoma South, atakapoweka jiwe la msingi ujenzi wa nyumba za gharama nafuu eneo la Muskoma Kanduyi.

Ziara hiyo ya Rais katika kaunti ya Bungoma inatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi wakuu serikalini kutoka eneo, hilo akiwemo Spika wa bunge la kitaifa Moses Wetang’ula.

Website | + posts