Home Habari Kuu Rais Ruto kuzindua mkakati wa G7 wa Baraza la Magavana

Rais Ruto kuzindua mkakati wa G7 wa Baraza la Magavana

0

Rais William Ruto siku ya Alhamisi anatarajiwa kuzindua mkakati wa Baraza la Magavana unaowaleta pamoja magavana 7 wanawake.

Mkakati huo unaongozwa na mwenyekiti wa Baraza la Magavana Ann Waiguru wa Kirinyaga, magavana Susan Kihika wa Nakuru, Wavinya Ndeti wa Machakos, Fatuma Achani wa Kwale, Kawira Mwangaza wa Meru na Cecily Mbarire wa Embu.

Unalenga kuwawezesha viongozi wanawake kudhihirisha uwajibikaji wao, kuleta mageuzi na kuwa na uongozi wenye mikakati mwafaka ya usimamizi.

Pia unaangazia kubuni miradi ya kuwaimarisha  wanawake katika kaunti hizo saba na kupigia debe kuongezewa nafasi za wanawake wateule katika siasa.

Website | + posts