Home Habari Kuu Rais Ruto kuongoza upanzi wa miti Kaunti ya Murang’a

Rais Ruto kuongoza upanzi wa miti Kaunti ya Murang’a

Aidha mawaziri na maafisa wakuu serikalini pia wataongoza shughuli hiyo ya upanzi wa miti kote nchini.

0
Rais William Ruto aongoza zoezi la upanzi wa miti.

Rais William Ruto leo Ijumaa ataongoza zoezi la kitaifa la upanzi wa miti, katika msitu wa Kiambicho ulioko Maragua, kaunti ya Murang’a.

Rais alitangaza Mei 10, 2024 kuwa siku ya upanzi wa miti, kuwakumbuka zaidi ya watu 250 waliofariki kutokana na mafuriko kote nchini.

Aidha mawaziri na maafisa wakuu serikalini pia wataongoza shughuli hiyo ya upanzi wa miti kote nchini.

Waziri mwenye mamlaka makuu Musalia Mudavadi, ataongoza shughuli hiyo katika kaunti za Tharaka  Nithi na Kirinyaga, huku mwanasheria mkuu Justin Muturi akiwa kaunti ya Bomet kwenye msitu wa Ndoinet.

Mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei anatarajiwa kuwa  Bomet, huku waziri wa uhifadhi wa mazingira Soipan Tuya akiongoza shughuli hiyo kwenye kaunti za Vihiga na Samburu.

Waziri wa habari na mawasiliano Eliud Owalo,atakuwa Nandi na Kisii, nao mawaziri  Kipchumba Murkomen na Davis Chirchir wakiongoza upanzi wa miti kwenye kaunti za Mombasa,Homa Bay,Baringo na Kericho.

Website | + posts