Home Habari Kuu Rais Ruto kuongoza mkutano wa baraza la usalama wa kitaifa kufuatia ajali...

Rais Ruto kuongoza mkutano wa baraza la usalama wa kitaifa kufuatia ajali ya ndege ya KDF

Katika ukurasa wake wa X Alhamisi jioni, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed alisema mkutano huo utajadili ajali hiyo ya ndege ya kijeshi iliyotokea Alhamisi alasiri.

0

Rais Wiliam Ruto ameitisha mkutano wa baraza la usalama wa taifa leo Alasiri, katika Ikulu ya Nairobi, kufuatia kuanguka kwa ndege ya vikosi vya ulinzi nchini KDF katika kaunti ya  Elgeyo-Marakwet.

Katika ukurasa wake wa X Alhamisi jioni, msemaji wa Ikulu Hussein Mohamed alisema mkutano huo utajadili ajali hiyo ya ndege ya kijeshi iliyotokea Alhamisi alasiri.

Ajali hiyo ilitokea Alhamisi alasiri, muda mfupi baada ya helikopta hiyo kung’oa nanga katika uwanja wa shule ya upili ya wavulana ya Cheptulel.

Maafisa wa KDF walikuwa katika shule hiyo kukadiria hali ya usalama, pamoja na mikakati iliyowekwa ya ufunguzi wa shule katika mpaka wa Pokot Magharibi na Marakwet.