Home Habari Kuu Rais Ruto kuongoza mkutano wa baraza la mawaziri Jumanne asubuhi

Rais Ruto kuongoza mkutano wa baraza la mawaziri Jumanne asubuhi

Rais Ruto alisema mkutano huo utajadili hatua za kuhakikisha kwamba wahasiriwa wa mafuriko wanashughulikiwa na serikali.

0

Huku maeneo mengi ya taifa hili yakiathirika na mafuriko kutokana na mvua kubwa inayonyesha, Rais William Ruto Jumanne asubuhi ataongoza mkutano wa baraza la mawaziri kujadili hatua zaidi za kukabili janga la mafuriko nchini.

Mkutano huo wa baraza la mawaziri, unajiri siku moja baada ya zaidi ya watu 50 kufariki Jumatatu alfajiri baada ya  kusombwa na maji mjini Maai Mahiu baada ya bwawa moja kuvunja kingo zake kutokana na mafuriko.

Akizungumza jana Jumatatu pembezoni mwa kongamano la kimataifa kuhusu maendeleo IDA21 katika jumba la mikutano ya Kimataifa KICC Jijini Nairobi, Rais Ruto alisema mkutano huo utajadili hatua za kuhakikisha kwamba wahasiriwa wa mafuriko wanashughulikiwa na serikali.

Mafuriko hayo yanayotokana na mvua kubwa, yamesababisha vifo vya mamia ya watu na uharibifu wa mali ya thamani ya mamilioni ya pesa.

Kulingana na msemaji wa serikali Isaac Mwaura, hadi kufikia jana Jumatatu jumla ya watu 169 walikuwa wamefariki kote nchini kutokana na athari za mafuriko.

Website | + posts