Home Kimataifa Rais Ruto kuongoza mkutano wa Baraza Kuu la UDA Ijumaa

Rais Ruto kuongoza mkutano wa Baraza Kuu la UDA Ijumaa

Habari kuhusu mkutano huo ilifichuliwa jana Alhamisi na Seneta wa kaunti ya Kericho ambaye pia ni mwanachama wa Baraza Kuu la chama hicho Aaron Cheruiyot.

0
Rais Ruto Kuongoza mkutano wa Baraza Kuu Jijini Nairobi.
kra

Rais William Ruto leo Ijumaa ataongoza mkutano wa Baraza Kuu la chama cha  UDA, kwenye makao makuu ya chama hicho jijini  Nairobi.

Mkutano huo unajiri baada ya kushuhudiwa malumbano katika Makao Makuu ya chama hicho, huku Joe Khalende akijitangaza yeye ndiye Katibu Mkuu wa chama hicho akidai kutimuliwa kwa Cleophas Malala katika wadhifa huo.

kra

Habari kuhusu mkutano huo ilifichuliwa jana Alhamisi na Seneta wa kaunti ya Kericho ambaye pia ni mwanachama wa Baraza Kuu la chama hicho Aaron Cheruiyot.

Akizungumza katika eneo la Belgut, kaunti ya Kericho, Cheruiyot alisema chama hicho kimejitolea kuhakikisha hakuna malumbano yanayoshuhudiwa tena kwenye chama hicho.

Mnamo siku ya Jumatano, wafuasi wa Malala waliandamana nje ya Makao Makuu ya chama hicho, wakipinga juhudi zozote za kumtimua Malala katika wadhifa huo.

Mkutano huo wa leo unalenga kutuliza joto katika chama hicho tawala.