Home Habari Kuu Rais Ruto kuhudhuria mahafala ya 87 ya makurutu 10,000 wa NYS

Rais Ruto kuhudhuria mahafala ya 87 ya makurutu 10,000 wa NYS

0

Rais William Ruto atahudhuria sherehe za 87 za kufuzu kwa makurutu wa shirika la huduma ya vijana kwa taifa, NYS zitakazoandaliwa katika chuo cha Gilgil leo Ijumaa.

Makurutu hao wanahitumu baada ya kupokea mafunzo ya miezi sita.

Maafisa wa NYS wanatarajiwa kunufaika pakubwa baada ya Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria kufichua kuwa maafisa wa NYS 3,000 wataajiriwa na kikosi cha polisi huku wengine 1,500 wakitarajiwa kuteuliwa kujiunga na idara ya polisi wa misitu.

Takriban makurutu 10,000 wanatarajiwa kufuzu kwenye mahafala ya Ijumaa.

Website | + posts