Home Habari Kuu Rais Ruto kuanzisha Safari Rally

Rais Ruto kuanzisha Safari Rally

0

Rais William Ruto anatarajiwa kuanzisha makala ya mwaka huu ya mashindano ya magari, maarufu kama WRC Safari Rally katika jumba la KICC kuanzia saa nne.

Makala ya mwaka huu ni ya nne tangu kurejeshwa kwa Safari Rally katika msururu wa dunia, na yanarejea katika kalenda yake ya kihistoria katika msimu wa Pasaka kwa mara kwanza tangu mwaka 1998.

Mashindano ya Kenya ni ya tatu katika msururu wa mashindano ya mwaka 2024 baada ya yale ya Monte Carlo na Uswidi.

Baada ya kuanzishwa Alhamisi, madereva wataelekea kituo cha kwanza cha mashindano eneo la Kasarani, maarufu kama Super Special Kasarani kuanzia saa nane adhuhuri.

Hapa, madereva watashindana umbali wa takriban kilomita 4.8.

Kituo cha Kasarani ndicho pekee ambacho madereva hushindana uso kwa uso kati ya vituo vyote 19.

Jumla ya madera 29 wa kimaitaifa watashindana kwenye mashindano hayo yatakayokamilika Jumapili.

Website | + posts