Home Kimataifa Rais Ruto: Kenya na Tanzania zimejitolea kuimarisha uhusiano

Rais Ruto: Kenya na Tanzania zimejitolea kuimarisha uhusiano

kra

Rais William Ruto amesema Kenya na Tanzania zimejitolea kuimarisha uhusiano kati yao kwa minajili ya ushirikiano wa kijamii na kiuchumi kwa manufaa ya watu wa nchi hizi mbili.

Rais aliyekuwa akiongea leo Ijumaa wakati wa maadhimisho ya miaka sitini ya muungano wa iliyokuwa jamhuri ya Tanganyika na jamhuri ya Zanzibar alisema nchi hizi mbili zina turathi sawa.

kra

Sherehe hiyo iliyoongozwa na Rais Samia Suluhu, iliandaliwa katika uwanja wa michezo wa kitaifa wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Sherehe hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi wa mataifa mengine wanachama wa jumuia ya maendeleo ya kusini mwa Afrika na jumuia ya Afrika mashariki.

Viongozi hao ni Rais Hakainde Hichilema wa Zambia, Evariste Ndayishimiye wa Burundi, Azali Assoumani wa Comoros, Nangolo Mbumba wa Namibia, Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, Felix Tshisekedi wa DRC na Hussein Ali Mwinyi wa Zanzibar.