Home Habari Kuu Rais Ruto: Kenya itaimarisha uhusiano wake na DRC

Rais Ruto: Kenya itaimarisha uhusiano wake na DRC

Rais William Ruto, alitoa hakikisho kwamba wananchi wa Kenya wataendeleza urafiki na jamhuri hiyo.

0
Rais William Ruto.

Kenya imesema itaimarisha uhusiano wa kidiplomasia na jamhuri ya kidemokrasia ya Congo-DRC, kwa manufaa ya raia wa mataifa haya mawili.

Rais William Ruto ambaye alihudhuria hafla ya kuapishwa kwa rais Félix Antoine Tshisekedi, alitoa hakikisho kwamba wananchi wa Kenya wataendeleza urafiki na jamhuri hiyo.

Rais Ruto alimpongeza rais Tshisekedi na kumtakia kila la heri anapoanza kipindi cha pili uongozini. Tshisekedi aliapishwa kwneye uwanja wa Martyrs jijini Kinshasa.

Alipata zaidi ya asilimia 70 ya jumla ya kura zilizopigwa kwenye uchaguzi mkuu wa mwezi Disemba mwaka uliopita.

Wakati huo huo Rais William Ruto kesho Jumapili, atahudhuria ibada ya maombi ya madhehebu mbalimbali katika uwanja wa shule ya msingi ya Machakusi kaunti ndogo ya Teso kaskazini katika kaunti ya Busia.

Kamishna wa kaunti hiyo Kipchumba Rutto, alisema kiongozi wa taifa akiandamana na maafisa wakuu serikali na viongozi wa eneo hilo, baadaye alasiri atazindua mradi wa maji wa Malaba-Malakisi huko Malakisi kweneye mpaka baina ya kaunti za Busia na Bungoma.

Mradi huo wa maji unalenga kukomesha tatizo la mara kwa mara la uhaba wa maji katika eneo la Teso kaskazini na viunga vyake.

Website | + posts
PCS
+ posts