Home Habari Kuu Rais Ruto: Kenya itaendeleza uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine

Rais Ruto: Kenya itaendeleza uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine

Rais Ruto alisema serikali itatumia uhusiano huo kutafuta fursa ambazo hazijatumiwa, na kupanua matarajio ya biashara na uwekezaji.  

0
Rais William Ruto awapokea mabalozi wapya katika Ikulu ya Nairobi.
kra

Kenya itaendeleza uhusiano wa kidiplomasia na mataifa mengine kwa manufaa ya raia wa taifa hili, hayo yamesemwa leo Jumatano na Rais William Ruto.

Akizungumza katika Ikulu ya Nairobi, baada ya kupokea stakabadhi kutoka kwa mabalozi sita wapya waliotumwa kuhudumu humu nchini, kiongozi wa taifa alisema kuwa taifa hili limejitolea kushirikiana na washirika wake katika kuendeleza ustawi wa kimataifa.

kra

Rais alisema Kenya iko makini kuvutia uwekezaji, kupanua masoko kwa bidhaa za humu nchini na kufungua nafasi za kiuchumi kwa vijana wa taifa hili.

Rais Ruto alisema serikali itatumia uhusiano huo kutafuta fursa ambazo hazijatumiwa, na kupanua matarajio ya biashara na uwekezaji.

Mabalozi hao ni pamoja na Anouar Ben Youssef (Tunisia), Patricio Alberto Aguirre Vacchieri (Chile), Luis Alejandro Levit (Argentina) na Romy Sonia Tincopa Grados (Peru).

Wengine ni  Sabit Subasic (Bosnia na Herzegovina) na Joan Thomas Edwards,(Jamaica).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here