Home Habari Kuu Rais Ruto: Jenerali Ogolla alifanya mabadiliko makubwa jeshini

Rais Ruto: Jenerali Ogolla alifanya mabadiliko makubwa jeshini

0
Rais William Ruto na mkuu wa vikosi vya ulinzi marehemu Jenerali Francis Ogolla.

Rais William Ruto, amemsifu mkuu wa vikosi vya ulinzi marehemu Jenerali Francis Ogolla, akisema alifanya mabadiliko makubwa katika kipindi kifupi ambacho alihudumu wadhifu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi.

kwa mujibu wa Rais, marehemu CDF iliunda harambee na mashirika mengine ya usalama ili kulinda usalama wa taifa.

Rais Ruto alisema chini ya uongozi wake, kulikuwa na visa vichache sana vya ugaidi nchini kwa sababu alikuwa mwerevu na alitoa uongozi bora.

“Ikiwa kuna uteuzi mmoja ambao nilifanya na ninajivunia sana, ni ule wa Jenerali Ogolla. Alikuwa mtaalamu na kiongozi,” alisema. “Tumepoteza mtu ambaye, naamini, angebadilisha jeshi letu.”

Alisema Jenerali Ogolla aliahidi kuhamasisha pesa na kusimamia kujegwa upya kwa shule katika Kerio Valley ambayo ina matatizo.

Alifariki akiwa kazini, Rais Ruto alieleza, alipokuwa akijibu kilio cha wanawake na watoto walioteswa na majambazi na wezi wa mifugo.

“Hivyo ndivyo Jenerali Ogolla aliiaminia nchi,” alisema.

Aliwataka Wakenya kuiga Jenerali Ogolla, akisema: “Kwa unyenyekevu wake, kuna mafunzo kwa ajili yetu sote.”

Atazikwa Jumapili nyumbani kwake Alego, Kaunti ya Siaya.

Website | + posts
PCS
+ posts