Home Habari Kuu Rais Ruto: Huduma Namba ilikuwa ulaghai mtupu

Rais Ruto: Huduma Namba ilikuwa ulaghai mtupu

0

Mpango wa Huduma Namba ulikuwa ulaghai mtupu uliosababisha kupotea kwa mabilioni ya fedha za umma bila sababu.

Takriban shilingi bilioni 15 zilitumiwa kwa mpango huo wakati wa utawala wa Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta huku Wakenya wakishurutishwa kujiandikisha.

“Sote tunajua kwamba kulikuwa na mradi ghushi ulioitwa Huduma Namba. Hiyo Huduma Namba ilikuwa ulaghai mtupu kwa sababu tulipoteza karibu shilingi bilioni 15 na kupata manufaa madogo mno kutokana na mradi huo,” alisema Rais Ruto wakati wa uzinduzi wa programu ya Gava Mkononi leo Ijumaa.

“Tunapaswa kudhihirisha katika kipindi cha siku 90 zijazo kwamba inawezekana kwetu sisi kuwa na utambulisho wa kidigitali bila kutumia shilingi bilioni 15 na bila kuwalaghai Wakenya,” aliongeza Ruto akisema wale waliohusika katika ulaghai huo wanapaswa kuabika.

Katika kipindi cha miezi mitatu ijayo, Ruto alisema nchi hii ni sharti iwe na utambulisho wa kidigitali.

Kadhalika aliagiza kwamba hakuna huduma yoyote ya serikali inapaswa kulipiwa kwa pesa taslimu.

Alisema, miongoni mwa mambo mengine, hatua hiyo itasaidia kukomesha ufisadi nchini.

Malipo yote ya serikali badala yake yatatolewa kupitia kwa namba ya paybill ambayo ni 222 222 itakayosimamiwa na Wizara ya Fedha.

Namba zingine zote za paybill zaidi ya 1,000 zilizotumiwa kulipia huduma za serikali zitafutiliwa mbali katika kipindi cha miezi mitatu ijayo.

 

 

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here