Wakenya sasa watapata huduma nafuu za afya kwa njia shwari na bila ubaguzi.
Hii baada ya kutiwa saini kwa miswada minne ya mageuzi ya Huduma za afya kwa wote siku ya Alhamisi na Rais William Ruto
Miswada hiyo ni pamoja na sheria ya afya ya msingi ya mwaka 2023, sheria ya afya ya kidijitali ya mwaka 2023, sheria ya fedha kuhusu vituo vya afya ya mwaka kuimarisha ya mwaka 2023 na sheria ya bima ya afya ya kijamii ya mwaka the Social Health ya mwaka 2023.
Sheria hizo zitatoa mikakati mwafaka ya kisheria ili kufanikisha utoaji wa huduma za afya kwa wote.
“Sheria hizi zitabadilisha mfumo wa huduma za afya nchini Kenya, zitaokoa maisha, zitaboresha jamii na kufanya taifa lenye nguvu na afya bora,” alisema Rais Ruto.
Kulingana na Rais sheria hizo zitasitisha changamoto zinazoghubika utoaji wa huduma za afya hapa nchini