Home Habari Kuu Rais Ruto azindua taasisi ya majani chai ya Lipton

Rais Ruto azindua taasisi ya majani chai ya Lipton

0

Rais William Ruto amezindua rasmi taasisi ya ubunifu na teknolojia ya maandalizi ya majani chai ya Lipton iliyoafikiwa kupitia ushirikiano kati ya kampuni ya majani chai ya Liptons na serikali kuu.

Lengo kuu la taasisi hiyo ya kwanza ya aina yake nchii ni kuboresha ujuzi katika utayarishaji wa majani chai humu nchini.

Rais Ruto alipongeza kampuni ya Liptons kwa mradi huo ambao anaamini utabadili kabisa sekta ya majani chai nchini Kenya.

Kampuni hiyo ya Lipton inaongoza katika uuzaji wa chai ya Kenya katika masoko ya kigeni na ina matawi yake huko Mombasa na Kericho.

Chini ya ushirikiano huo, kampuni ya Liptons imetakiwa kutambua Kenya kuwa chimbuko la chai inayouza ulimwenguni katika nembo zake.

Lengo la serikali kulingana na Rais Ruto ni kurejesha Kenya katika hadhi yake ya awali kama mzalishaji mkuu wa chai na hatimaye kuongezea wakulima wa zao hilo mapato kando na kupanua fursa zilizopo za kiuchumi katika sekta ya chai.

Taasisi ya Lipton Tea Innovation and Technology Academy iko katika chuo kikuu cha Kabianga kilicho katika kaunti ya Kericho lakini uzinduzi ulifanyika katika Ikulu ya Nairobi.

Wakulima wa majani chai watapokea mafunzo kuhusu kuboresha kilimo chao katika taasisi hiyo.

Website | + posts