Home Biashara Rais Ruto azindua mradi wa uunganishaji umeme Murang’a

Rais Ruto azindua mradi wa uunganishaji umeme Murang’a

0
kra

Rais William Ruto leo Ijumaa amezindua mradi wa uunganishaji umeme wa Last Mile katika kijiji cha Kirungu mjini Kiriaini katika kaunti ya Murang’a. 

Mradi huo unalenga kuhakikisha kaya 15,000 katika eneo hilo zina umeme.

kra

“Upanuzi wa usambazaji wa umeme humu nchini kupitia mpango wa uunganishaji umeme wa Last Mile utawahakikishia wafanyabiashara wadogo wadogo umeme wa kutegemewa na kuongeza ushindani na mapato yao,” alisema Rais Ruto wakati wa uzinduzi huo.

Rais pia alizindua ujenzi wa barabara ya kilomita 20 ya Kiriaini-Mugeka ambayo inakusudia kurahisisha usafiri katika eneo bunge la Mathioya.

Alifanya uzinduzi huo akiwa ameandamana na Naibu wake Rigathi Gachagua na Waziri wa Nishati Opiyo Wandayi miongoni mwa maafisa wengine.

Website | + posts