Raia Wiliam Ruto Ijumaa jioni aliwasili Jijini Bulawayo, Zimbabwe kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili.
Rais Ruto ambaye ameandamana na mama taifa Rachel Ruto, alilakiwa na mwenyeji wake Emmerson Mnangagwa, katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Joshua Mquabuko Nkomo.
Kiongozi wa taifa atakuwa mgeni wa heshima katika maonyesho ya 64 ya Jijini Bulawayo Leo Jumamosi.
Kupitia kwa taarifa, ikulu ya Nairobi ilisema ziara hiyo inalenga kuimarisha uhusiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya Nairobi na Zimbabwe.