Home Habari Kuu Rais Ruto awasili Uswizi kwa mkutano wa amani kati ya Ukraine na...

Rais Ruto awasili Uswizi kwa mkutano wa amani kati ya Ukraine na Urusi

Kongamano hilo linalenga kubuni mikakati ya kwanza kuleta udhabiti katika taifa hilo la mashariki mwa bara Ulaya.

0
Rais William Ruto awasili Uswizi.
kra

Rais William Ruto amewasili Jijini Bürgenstock, Uswizi, kuhudhuria mkutano wa ngazi ya juu kuhusu juhudi za kuleta amani nchini Ukraine.

Kongamano hilo linalenga kubuni mikakati ya kwanza ya kuleta udhabiti katika taifa hilo la mashariki mwa bara Ulaya.

kra

Washiriki wa mkutano huo wa Jumamosi na Jumapili, utajadili mapendekezo 10 yaliyotolewa na Ukraine ili kusitisha vita kati ya nchi hiyo na Urusi.

Rais Ruto anatarajiwa kuhutubia mkutano huo, huku akiangazia vita katika mashariki ya kati na Afrika.

Kiongozi huyo wa taifa pia atapigia kurunzi vita vilivyosahaulika barani humu, na athari zake katika ukuaji wa uchumi.

Zaidi ya viongozi 100 wa nchi na serikali wanahudhuria mkutano huwa wa siku mbili.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here