Home Habari Kuu Rais Ruto awaonya wanaosambaza mbolea bandia

Rais Ruto awaonya wanaosambaza mbolea bandia

Rais alisema ataendelea kushinikiza kupunguzwa zaidi kwa bei ya mbolea, ili kuhakikisha wakulima wanapata faida zaidi.

0
Rais William Ruto awaonya wanaosambaza mbolea feki.

Rais William Ruto amesema wanaosambaza mbolea bandia watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Akiongea leo Jumatatu baada ya kufanya ziara katika ghala ya Halmashauri ya Nafaka na Mazao, NCPB mjini Eldoret, kiongozi wa taifa alisema ameridhika na shughuli ya usambazaji mbolea ya bei ya bei nafuu inayotekelezwa na halmashauri hiyo.

Hata hivyo, Rais alisema mchakato wa usambazaji mbolea hiyo unapaswa kuongezwa kasi, ikizingatiwa kuwa sehemu nyingi za nchi zinashuhudia msimu wa mvua.

Rais alisema ataendelea kushinikiza kupunguzwa zaidi kwa bei ya mbolea ili kuhakikisha wakulima wanapata faida zaidi.

Aliwahakikishia wakulima wote kote nchini kwamba kuna mbolea ya kutosha kukidhi mahitaji yao.

Alisema amejitolea kuhakikisha uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa watu wote hapa nchini.

‚ÄúTunapunguza bei ya pembejeo za kilimo ili kukabiliana na baa la njaa,” alisema Rais Ruto.

Website | + posts