Home Kimataifa Rais Ruto awaomboleza waliofariki mkurupukoni Kericho

Rais Ruto awaomboleza waliofariki mkurupukoni Kericho

0
kra

Rais William Ruto amewaomboleza watu wanne waliofariki wakati wa mkurupuko uliotokea katika uwanja wa michezo wa Kericho yalikofanyika maadhimisho  ya miaka 60 ya Siku ya Mashujaa. 

Wizara ya Usalama wa Kitaifa inasema watu wote waliofariki walikuwa wanawake.

kra

Watu wengine 10 walijeruhiwa wakati wa kisa hicho kilichotokea saa tisa alfajiri leo Ijumaa, wanne wakiwa raia na sita maafisa wa polisi.

“Natuma rambirambi zangu za dhati kwa familia za waathiriwa wa mkasa uliotokea katika Uwanja wa Kericho Green kabla ya sherehe za Siku ya Mashujaa. Tunatuma pole zetu za dhati na kuwatakia waliojeruhiwa nafuu ya haraka. Poleni sana,” alisema Rais Ruto kupitia mtandao wake wa X.

Katika taarifa, Wizara ya Usalama wa Kitaifa imesema hali ya waliojerujiwa ni thabiti na kwamba wanaendelea kupata matibabu katika hospitali ya rufaa ya Kericho.

Aidha miili ya waliofariki imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali hiyo ikisubiri kutambuliwa na kufanyiwa upasuaji.

“Tunaomba ushirikiano na utulivu kutoka kwa umma tunapofanya uchunguzi wa kubaini hali zilizochochea kutokea kwa tukio hili lililosababisha vifo na kuhakikisha hatua zinachukuliwa kuzuia kutokea kwa matukio kama hayo siku za usoni,” ilisema taarifa ya Wizara ya Usalama wa Kitaifa.

Website | + posts