Home Habari Kuu Rais Ruto awahamisha Makatibu wa Wizara

Rais Ruto awahamisha Makatibu wa Wizara

0

Rais William Ruto siku ya  Jumatano alifanya mabadiliko katika Makatibu wa Wizara kwa lengo la kuimarisha utendakazi wa serikali ya Kenya kwanza.

Katika mabadiliko hayo, Veronica Nduva amehamishwa kutoka Wizara ya Jinsia hadi Idara ya Utendakazi na Usimamizi wa Utoaji Huduma.

Harsama Kello sasa ni Katibu katika Wizara ya Maeneo Kame na Maendeleo ya Kanda. Awali, Kello alikuwa Katibu katika Idara ya Ustawi wa Kilimo chini ya Wizara ya Kilimo.

Julius Korir sasa ndiye Katibu katika Idara ya Maji na Usafi huku Paul Rono akiteuliwa kuwa Katibu katika Idara ya Ustawi wa Kilimo.

Idris Salim Dokota amehamishwa kuwa Katibu katika Idara ya Masuala ya Baraza la Mawaziri. Awali, Dokota alikuwa Katibu katika Idara ya Maeneo Kame na Maendeleo ya Kanda.

Katika mabadiliko hayo, Ann Wang’ombe sasa ndiye Katibu katika Idara ya Jinsia huku Shadrack Mwadime akiteuliwa Katibu katika Idara ya Leba na Ukuzaji Ujuzi.

Geoffrey Kaituko amehamishwa hadi Idara ya Safari za Meli na Masuala ya Baharini. Kaituko alikuwa Katibu katika wizara ya Leba na Ukuzaji Ujuzi kabla ya kufanywa kwa mabadiliko hayo ambayo yanaanza kutekelezwa mara moja.

Website | + posts