Rais William Ruto ametangaza kuvunjilia mbali mashirika 47 ya serikali, kama njia ya kupunguza matumizi ya pesa.
Akitangaza hayo Ijumaa kwenye Ikulu ya Nairobi, Ruto amesema wafanyikazi hao wa mashirika yatakayovunjwa watahamishiwa kwingine.
Aidha Ruto ametangaza kupunguza bajeti ya idara zote za serikali, huku afisi yake ikipunguziwa bajeti kwa asilimia 15.