Home Kimataifa Rais Ruto atuma risala za rambirambi kwa raia wa Ethiopia

Rais Ruto atuma risala za rambirambi kwa raia wa Ethiopia

Hadi kufikia sasa maporomoko hayo ya ardhi yamesababisha vifo vya watu 257, huku zaidi ya watu 15,000 wakiathiriwa.

0
Maporomoko ya ardhi yakumba kusini mwa Ethiopia.
kra

Rais William Ruto ametuma risala za rambirambi kwa raia wa Ethiopia, kufuatia maporomoko ya ardhi yaliyosababisha maafa katika eneo la Gozdi Kebele.

Katika risala hizo, kiongozi huyo wa taifa alimhakikishia Waziri Mkuu wa Ethiopia kuwa Kenya iko tayari kumshika mkono wakati huu mgumu wa janga hilo.

kra

“Mawazo yetu yako na raia wa Ethiopia huku tukiombea familia zilizoathirika,” alisema Rais Ruto.

Hadi kufikia sasa maporomoko hayo ya ardhi yamesababisha vifo vya watu 257, huku zaidi ya watu 15,000 wakiathiriwa.

Rais Ruto alipongeza utawala wa ndani wa taifa hilo, shirika la msalaba mwekundu nchini humo na asasi zote za serikali ya Ethiopia kwa juhudi zao za kuwatafuta na kuwaokoa manusura.

Maporomoko hayo ya ardhi yalitokea siku ya Jumapili jioni na Jumatatu asubuhi juma hili, baada ya mvua kubwa kunyesha katika eneo lenye milima la Gofa, kusini mwa Ethiopia.

Eneo la kusini mwa Ethiopia limekumbwa na mvua kubwa na mafuriko katika miezi ya hivi karibuni.