Home Habari Kuu Rais Ruto atoa ujumbe wa pole kwa kiongozi na watu wa Abu...

Rais Ruto atoa ujumbe wa pole kwa kiongozi na watu wa Abu Dhabi

0
Sheikh Tahnoon

Rais William Ruto ametoa ujumbe wa pole kwa kiongozi na watu wa Abu Dhabi kufuatia kifo cha mwakilishi wa kiongozi wa Abu Dhabi katika eneo la Al Ain.

Rais alisema alisikitishwa sana na habari za kifo cha Sheikh Tahnoon bin Mohammed Al Nahyan na kwa niaba ya serikali na watu wa Kenya anasema pole.

Ujumbe wake ulielekezwa kwa Rais wa UAE ambaye pia ni kiongozi wa Abu Dhabi Sheikh Mohamed bin Zayed Al Nahyan, kwa familia nzima ya Al Nahyan na watu wa UAE.

Alisema marehemu Sheikh Tahnoun atakumbukwa kwa jukumu lake muhimu katika kuanzishwa kwa umoja wa milki za kiarabu kwa kushirikiana na mwanzilishi wake Sheikh Zayed na hatimaye muungano huo ukabuniwa rasmi Disemba 2, 1971.

“Naomba Mungu aipe familia ya Al Nahyan nguvu wanapopambana na msiba huu.” alisema Rais Ruto kwenye taarifa.

Sheikh Tahnoon aliaga dunia Mei Mosi, 2024 akiwa na umri wa miaka 82 na serikali ya UAE ikatangaza siku 7 za maombolezi ya kitaifa.

Website | + posts