Home Habari Kuu Rais Ruto atia Saini mswada wa ugavi wa mapato kuwa sheria

Rais Ruto atia Saini mswada wa ugavi wa mapato kuwa sheria

0

Rais William Ruto leo Ijumaa, ametia saini kuwa sheria Mswada wa Ugavi wa Mapato kwa Kaunti wa 2023 na pia Mswada wa Hazina ya Usawazishaji wa 2023.

Miswada hiyo miwili itawezesha magatuzi 47 kupata fedha katika mwaka mpya wa kifedha unaoanza kesho.

Sheria ya Mapato ya Kaunti inatenga shilingi bilioni 385.4 za kugawa magatuzi.

Sheria ya Ugavi wa mapato kwa magatuzi hutenga shilligi millioni 385.4 za ugavi huo.

Serikali ya kaunti ya Nairobi itapata mgao zaidi wa shillingi billioni 20.07.

Mswada wa sheria ya fedha za usawasishaji inatenga shillingi billioni 10.3 kwa matumizi ya kawaida kama vile, maji, barabara, umeme na afya kwa maeneo yaliotengwa nchini.

Waliohudhuria shughuli hiyo ni pamoja na naibu rais Rigathi Gachagua miongoni mwa viongozi wengine.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here