Home Habari Kuu Rais Ruto atangaza shule kufunguliwa Mei 13

Rais Ruto atangaza shule kufunguliwa Mei 13

Rais alitangaza hayo alipokutana na viongozi kutoka kaunti za Laikipia na Kajiado katika Ikulu ya Nairobi.

0
Rais William Ruto.

Rais William Ruto leo Jumatano, ametangaza kuwa  shule zitafunguliwa kwa muhula wa pili Jumatatu Mei,13, 2024.

Rais alitangaza hayo alipokutana na viongozi kutoka kaunti za Laikipia na Kajiado katika Ikulu ya Nairobi.

Kulingana na Rais, fedha za ukarabati wa shule zilizoathiriwa na mafuriko, zitatolewa kupitia hazina ya ustawi wa maeneo bunge NG-CDF.

Kiongozi wa taifa alisema uamuzi huo unafuatia ushauri wa idara ya utabiri wa hali ya anga kwamba mvua ya bojo ambayo imekuwa ikishuhudiwa imepungua.

Awali tarehe ya kufunguliwa kwa shule ilikuwa Aprili 29,2024, lakini ufunguzi huo ukaahirishwa hadi Mei 6,2024, kufuatia mafuriko ambayo yamekumba maeneo mengi  ya nchi.

Hata hivyo siku ya Ijumma iliyopita, Rais aliagiza kwamba shule zisalie zimefungwa kwa muda ambao haukubainishwa kufuatia mafuriko ambayo yamesababisha vifo vya watu wapatao 238 kufiikia sasa.

Website | + posts