Rais William Ruto ametaka uchunguzi wa haraka kufuatia vifo vya zaidi ya wanafunzi 21, katika shule ya Hillside Endarasha Academy katika mkasa wa moto wiki iliyopita.
Ruto ameamrisha wizara ya usalama wa kitaifa na ile ya elimu kuharakisha uchunguzi unaoendelea na kuhakikisha masharti yaliyowekwa kwa shule za malazi kwa wanafunzi yanazingatiwa.
Watoto hao waliangamia kwenye mkasa wa moto ulioteketeza bweni walimolala Alhamisi iliyopita.
Ruto amesema haya baada ya kukutana na Mawaziri na makatibu wa wizara hizo mbili Jumatatu alasiri.