Home Habari Kuu Rais Ruto asema yuko tayari kujadiliana na Raila Odinga

Rais Ruto asema yuko tayari kujadiliana na Raila Odinga

0
Rais William Ruto.

Kiongozi wa nchi ya Kenya Rais William Ruto amesema kwamba yuko tayari kwa majadiliano na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Haya yanajiri muda mfupi baada ya Raila kwenye kikao na wanahabari wa kimataifa kudai kwamba juhudi za kutafuta majadiliano na Rais Ruto kuhusu matatizo yanayowakumba wakenya hazijafanikiwa.

Kupitia kitandazi cha Twitter Rais alimwambia Raila ambaye alimrejelea kama rafiki kwamba anaelekea Tanzania Kwa mkutano kuhusu raslimali watu na kupanua nafasi za ajira barani Afrika. Alisema anarejea jioni ya leo na yuko tayari kukutana naye.

Kwenye kikao na wanahabari, Raila alitambua kwamba tatizo la gharama ya juu ya maisha sio la Kenya pekee lakini serikali ya Kenya Ina uwezo wa kupunguzia wakenya mzigo.

Aliwalaumu maafisa wa polisi kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji waliokuwa wakionyesha kukerwa kwao na gharama ya maisha.

Waziri wa mambo ya ndani Kithure Kindiki hata hivyo alikanusha madai ya maafisa wa polisi kuhusika kwenye mauaji au kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya raia.

Alisema maafisa wa usalama hawaegemei upande wowote, hawana upendeleo na hutekeleza kazi yao ipasavyo kwa hivyo hawapaswi kuingizwa kwenye mivutano ya kisiasa, kikabila au mingine.

Website | + posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here