Home Habari Kuu Rais Ruto asema operesheni imerejesha utulivu North Rift

Rais Ruto asema operesheni imerejesha utulivu North Rift

0

Rais William Ruto amesema kwamba utulivu umerejea katika eneo la kaskazini mwa bonde la ufa kufuatia operesheni ya kiusalama iliyoanzishwa humo yapata mwaka mmoja uliopita.

Alisema kwamba visa vya hivi majuzi vya ujambazi na wizi wa mifugo katika eneo hilo vinashughulikiwa na maafisa wa usalama ambao wanatumia mbinu mpya.

“Tumejitolea kuhakikisha amani na usalama vinarejea katika eneo la North Rift na sehemu nyingine za nchi ambazo zimeshuhudia kuvurugwa kwa amani na usalama,” alisema Rais.

Aliyasema haya baada ya mkutano na wasimamizi wakuu wa usalama nchini kuhusu hali katika eneo la North Rift ambapo alifahamishwa kuhusu inavyoendelea “Operation Maliza Uhalifu”.

Waliohudhuria mkutano huo katika makazi ya Rais huko Kilgoris kaunti ya Narok ni Waziri wa Usalama wa Taifa Kithure Kindiki, Katibu wa Usalama wa Taifa Raymond Omollo, Inspekta Jenerali wa Polisi Japhet Koome, manaibu wake wawili Douglas Kanja na Noor Gabow, kamishna wa eneo la Rift Valley Abdi Hassan na kamanda wa polisi wa eneo hilo Tom Odero.

Website | + posts