Home Kimataifa Rais Ruto asema mpango wa Tumaini umepiga hatua kubwa

Rais Ruto asema mpango wa Tumaini umepiga hatua kubwa

0
kra

Rais William Ruto amesema kwamba mpango wa amani nchini Sudan Kusini kwa jina “Tumaini” umepiga hatua kubwa kutokana na uongozi na uzalendo wa wadau wote.

Akizungumza katika ikulu ya Nairobi alipopokea ripoti kuhusu unavyoendelea mpango huo, Rais alisema kwamba Kenya inatizamia wakati ambapo watu wa Sudan Kusini wataishi kwa amani, watakuwa salama na ustawi.

kra

Mpango huo almaarufu “Tumaini Peace Initiative” ulizinduliwa Mei 9, 2024 jijini Nairobi na lengo lake ni kutafuta amani ya kudumu nchini sudan Kusini kwa kuhusisha makundi yote ya nchi hiyo ambayo hayakutia saini makubaliano ya mwaka 2018.

Makubaliano ya mwaka 2018 yalilenga kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.

Wanaoongoza mpango wa Tumaini ni pamoja na Rais william Ruto ambaye ni mpatanishi mkuu, Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na aliyekuwa kamanda wa jeshi la Kenya meja jenerali Lazarus Sumbeiywo.

Wakati wa uzinduzi wa mpango huo, marais, wanadiplomasia na maafisa wakuu wa serikali mbali mbali barani Afrika walikuwepo kujionea kile kinachoaminika kuwa jaribio la mwisho la kurejesha amani nchini Sudan Kusini.

Baada ya mashauriano ya kina kuhusu utatuzi wa mizozo, Mei 16, 2024, wadau wote waliohudhuria walitia saini tamko la kujitolea kama njia ya kuahidi utayari wao kukataa vurugu za aina yoyote.

waliokuwepo ikulu kumjuza Rais Ruto ulikofikia mpango huo ni pamoja na Jenerali Lazarus Sumbeiywo, Jenerali Pagan Amum Okiech, Jenerali Paul Malong Awan, Jenerali Mario Loku Thomas Jada na Lual Dau.

Website | + posts