Home Habari Kuu Rais Ruto apokea mwaliko kuzuru Marekani

Rais Ruto apokea mwaliko kuzuru Marekani

Kulingana na ikulu ya Rais ya Marekani, ziara hiyo itatumika kuadhimika miaka 60 ya ushirikiano kati ya Kenya na Marekani.

0
Rais Ruto kuzuru Marekani mwezi Mei.

Rais wa Marekani Joe Biden na mkewe Jill Biden watakuwa wenyeji wa rais William Ruto na mkewe Mama Rachel Ruto, kwenye ziara rasmi nchini Marekani mwezi Mei mwaka huu.

Kulingana na ikulu ya Rais ya Marekani, ziara hiyo itatumika kuadhimika miaka 60 ya ushirikiano kati ya Kenya na Marekani.

“Ziara hiyo itaimarisha kujitolea kwetu kuhakikisha usalama na amani, itapanua ushirikiano wetu wa kiuchumi na kutetea demokrasia. Viongozi hao watajadiliana kuhusu kuhusu ushirikiano wa kibiashara, uwekezaji na uvumbuzi wa kiteknolojia, hali ya hewa, kawi safi, afya na usalama,” ilisema taarifa hiyo ya White House.

Huku akipokea mwaliko huo, Rais William Ruto alielezea shukrani zake, akisema ziara hiyo itatumika kusherehekea miongo sita ya ushirikiano wa kidiplomasia baina ya kenya na Marekani.

“Kwa niaba ya watu na serikali ya Kenya, namshukuru Rais na Mama taifa wa Marekani, kwa kunialika nchini humo kwa ziara ya kiserikali mwezi Mei 23, 2024,” alisema Rais Ruto.

Alisema anatarajia mazungumzo baina yake na rais Biden kuhusu maswala kadhaa ya umuhimu kwa mataifa hayo mawili sio tu maswala ya kiuchumi, siasa na diplomasia bali pia kujitolea kwa mataifa hayo mawili kwa maadili ya kimsingi ambayo yanafafanua ujumuishaji dhabiti wa sera na upatanishi wa kibiashara.

“Natazamia kujadiliana na Rais Biden kuhusu maswala kadhaa ya umuhimu kati  ya nchi hizi mbilki, sio tu kuhusu sekta ya uchumi, siasa na diplomasia, lakini kuhusu maadili muhimu ya biashara zetu watu na serikali,” alisema Rais Ruto.

Rais Ruto aidha alisema ziara hiyo itatoa fursa ya kuelezea enzi mpya ya ushirikiano unaolenga uwekezaji kwenye biashara, nishati safi, shughuli za kukabili mabadiliko ya tabia-nchi na teknolojia ya dijitalia na ubunifu.

Website | + posts