Rais William Ruto ametoa wito wa kufanyiwa mageuzi taasisi za kimataifa za ufadhili, akitetea mfumo wa ushirikishwaji zaidi.
Rais Ruto alisisitiza haja ya kuwepo demokrasia katika bodi za benki za maendeleo za kimataifa, ili kuhakikisha wanachama wote wana sauti sawa katika usimamizi wa taasisi hizo.
Kiongozi wa taifa alisema mfumo wa sasa wa kifedha hautekelezi hakii na unapuuza maslahi ya nchi zinazoendelea.
Aidha, rais alieleza bayana kwamba,hatua hiyo itaondolea mataifa mengi milundiko ya madeni,na kuwapa fursa ya kufikia malengo yao kimaendeleo.
Rais alisisitiza haja ya kutenga fedha za kusaidia kukabili kero la tabianchi,kuongeza thamani ya bidhaa na kuimarisha uagizaji na vile vile kutekeleza mwafaka wa soko huru barni Afrika ili kuboresha biashara baina ya mataifa ya Kiafrika.
Aliyasema hayo Ijumaa katika mkutano wa maafisa wakuu wasimamizi wa Afrika mwaka 2024 Jijini Kigali, Rwanda,