Home Habari Kuu Rais Ruto aongoza mkutano wa UDA

Rais Ruto aongoza mkutano wa UDA

0

Rais William Ruto leo Jumanne anaongoza mkutano wa Kamati Kuu ya Kitaifa ya chama cha UDA. 

Mkutano huo unafanyika katika makao makuu ya chama hicho jijini Nairobi.

Miongoni mwa masuala yanayotarajiwa kupewa kipaumbele wakati wa mkutano huo ni uchaguzi wa mashinani wa chama hicho ambao umeahirishwa mara kadhaa sasa.

Kumekuwa na shinikizo la kutaka kuvunja vyama tanzu vya muungano wa Kenya Kwanza ambao UDA ni mwanachama na badala yake kuunda chama kimoja.

Hata hivyo, ripoti zinaashiria kuwa vyama tanzu kama vile kile cha ANC chake kinara wa mawaziri Musalia Mudavadi na Ford K chake Spika wa Bunge la Taifa Moses Wetang’ula vimekataa jitihada hizo.

Haijabainika ikiwa uvunjaji wa vyama hivyo ni miongoni mwa masuala yatakayojadiliwa wakati wa mkutano wa UDA.