Home Taifa Rais Ruto aongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri

Rais Ruto aongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri

0
kra

Rais William Ruto leo Jumanne ameongoza mkutano wa Baraza la Mawaziri katika Ikulu ya Nairobi.

Huo ndio mkutano wa kwanza wa Baraza la Mawaziri kufanyika tangu kuundwa kwa serikali jumuishi.

kra

Mkutano huo ulihudhuriwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua miongoni mwa mawaziri wapya waliotajwa kwenye baraza hilo.

Miongoni mwao ni Waziri wa Fedha John Mbadi.

Mkutano huo unakuja wakati ambapo mjadala kuhusu mpango wa kukodi Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, JKIA kwa mfanyabiashara Adani umeshika kasi nchini.

Mpango huo umepingwa vikali na wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, KAA kwa hofu kwamba huenda wakapoteza kazi zao.

Aidha, Mawaziri wamekutana wakati ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wamepinga vikali mfumo mpya wa kufadhili masomo ya vyuo vikuu na taasisi zingine za elimu ya juu.

Baadhi wamedai waliwekwa kwenye makundi yasiyostahiki ya ufadhili yanayokinzana na hali ya kiuchumi ya familia wanazotoka.

Hata hivyo, tutakuletea taarifa za kina kuhusu yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri punde baada ya kuzipokea taarifa hizo.

Website | + posts