Home Habari Kuu Rais Ruto amteua Prof. Patrick Verkooijen kuwa chansela mpya wa chuo kikuu...

Rais Ruto amteua Prof. Patrick Verkooijen kuwa chansela mpya wa chuo kikuu cha Nairobi

Prof. Patrick Verkooijen kuwa chansela mpya wa chuo kikuu cha Nairobi.

0

Rais William Ruto amemteua Prof. Patrick Verkooijen kuwa chansela mpya wa chuo kikuu cha Nairobi kwa kipindi cha miaka mitano.

Prof. Verkooijen ni mwanamazingira mashuhuri aliye na ujuzi na utaalamu wa hali ya juu.

Prof Patrick V. Verkooijen amemrithi Dky. Vijoo Rattansi, aliyehudumu katika chuo hicho kikuu kwa miaka 10.

Prof Verkooijen, aliye pia afisa mkuu wa kituo cha kimataifa kuhusu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga amekuwa chansela wa kwanza wa taasisi hiyo kutoka nje ya bara Afrika.

Ataanza kutekeleza wadhifa huo rasmi tarehe mosi mwezi ujao. Rais Ruto alielezea furaha yake kwamba Prof Verkooijen ataongoza chuo hicho kikuu akisema ana ujuzi wa hali ya juu.

Chansela huyo mpya ana mtandao mkubwa katika ustawi wa elimu na rekodi thabiti kuhusu kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga na shughuli za kiuchumi zinazohifadhi mazingira.

Chansela huyo anatarajiwa kutumia ujuzi huo kuimarisha hadhi ya chuo hicho kama kituo cha viwango vya hali ya juu ya elimu.

Prof. Verkoojein ni mmojawapo wa waratibu wa mpango wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga barani Afrika, unaotekelezwa kwa pamoja na benki ya maendeleo barani Afrika na kituo cha kimataifa kuhusu kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya anga.

Mpango huo unaolenga kukusanya dola bilioni 25, kuharakisha na kuimarisha hatua za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga barani Afrika.

Website | + posts
PCS
+ posts