Home Kimataifa Rais Ruto amteua Dorcas Oduor kuwa Mwanasheria Mkuu

Rais Ruto amteua Dorcas Oduor kuwa Mwanasheria Mkuu

Iwapo ataidhinishwa na bunge,Oduor atakuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa Mwanasheria Mkuu hapa nchini.

0
Mwanasheria Mkuu mteule Dorcas Oduor.
kra

Rais William Ruto leo Jumanne amemteua Dorcas Odour kuwa Mwanasheria Mkuu, siku chache baada ya kubatilisha uteuzi wa Rebecca miano.

Uteuzi huo unajiri baada ya Rais William Ruto kutimua Baraza la Mawaziri pamoja na Mwanasheria Mkuu mnamo Julai 11,2024.

kra

Katika barua iliyotiwa saini na mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei, Oduor alitajwa kuwa na tajiriba ya uanasheria ya miaka 30 katika utumishi wa umma.

Iwapo ataidhinishwa na bunge katika wadhifa huo, Oduro atachukua nafasi iliyoshikiliwa na Justin Muturi ambaye sasa ameteuliwa kuwa waziri wa utumishi wa umma.

Oduor atakuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa wa Mwanasheria Mkuu hapa nchini.

Oduor atakuwa mshauri mkuu wa serikali, na atawakilisha serikali ya taifa mahakamani au katika kesi yoyote ambapo serikali inahusishwa.

Rais Ruto pia amemteua Beatrice Askul Moe kuwa waziri wa maswala ya Afrika mashariki na maendeleo ya kanda.