Home Kimataifa Rais Ruto akutana na mtoto Tinsley Nduta

Rais Ruto akutana na mtoto Tinsley Nduta

0
kra

Rais William Ruto alikutana na mtoto kwa jina Tinsley Nduta katika ikulu ya Nairobi jana Jumapili Mei 19, 2024. Nduta alikuwa ameandamana na wazazi wake baba George Ngugi, mama Agnes Wairimu na dadake Maureen Wambeti kwenye ziara hiyo ya ikulu.

Mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi ya Lizzie Wanyoike alipata umaarufu mitandaoni kupitia video ambapo alionyesha uvivu wa kurejea shuleni kwa muhula wa pili.

kra

Rais ruto alizungumza na Nduta kwa njia ya simu akamhimiza akubali kurejea shuleni akisema elimu ni muhimu, wazo alilorejelea jana wakati alikuwa mwenyeji wa Nduta.

“Alibadili mawazo kuhusu kurejea shuleni baada ya mazungumzo tuliyokuwa nayo wiki jana.” alisema Rais kwenye taarifa akiongeza kusema kwamba elimu hutekeleza jukumu muhimu katika kuunda mwelekeo wa maisha ya watoto na huwatayarisha kwa majukumu muhimu watakayotekeleza katika jamii siku za usoni.