Home Habari Kuu Rais Ruto akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Dubai

Rais Ruto akutana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Dubai

0

Rais William Ruto amekutana na Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Dunia Anne Bjerde mapema Ijumaa mjini Dubai, anakohudhuria mkutano wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi, COP28.

Ruto anajiunga na viongozi wengine ulimwenguni walio Dubai kuhudhuria mkutano huo ulioanza Novemba 30 na utakamilika Disemba 12.

Ruto ameandamana na Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi na Waziri wa Fedha Prof. Njuguna Ndung’u miongoni mwa viongozi wengine wakuu serikalini.

Website | + posts