Home Biashara Rais Ruto akutana na Katibu Mkuu wa UNCTAD

Rais Ruto akutana na Katibu Mkuu wa UNCTAD

0

Rais William Ruto amepongeza wajibu unaotekelezwa na Kamati ya Biashara na Maendeleo ya Umoja wa Mataifa (UNCTAD) katika kusaidia kuangazia changamoto kuu zinazokumba mataifa yanayostawi.

Rais Ruto amesema changamotoo hizo zinazuia maendeleo jumuishi, thabiti, yenye usawa na endelevu.

Aliongeza kuwa biashara inasalia nguzo muhimu kwa ukuaji endelevu wa kiuchumi na maendeleo ya muda mrefu.

“Kwa hivyo, tunahitaji kuunganisha jitihada zetu ili kuendelea kuchochea hili kwani Afrika ina rasilimali zinazohitajika na hivyo matumizi mazuri ya biashara yanaweza yakachochea maendeleo na kubuni manufaa mengi kabisa,” alisema Ruto.

Alitoa kauli hizo leo Jumanne katika Ikulu Ndogo ya Eldoret, kaunti ya Uasin Gishu, alipofanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa UNCTAD Rebeca Grynspan.

Walikutana siku moja kabla ya kuandaliwa kwa mkutano wa UNCTAD kesho Jumatano jijini Nairobi.

Rais Ruto aliyeandamana na Waziri wa Biashara Moses Kuria alipongeza kamati hiyo kwa kuichangua Kenya kama eneo la kuzinduliwa kwa ripoti ya kwanza ya UNCTAD.

Kichwa cha ripoti hiyo ni “Maendeleo ya Kiuchumi barani Afrika,” huku kaulimbiu yake ikiwa ‘uwezo wa Afrika wa kutumia mitungo ya usambazaji inayotumia teknolojia ya hali ya juu duniani’.

Waliokuwapo ni pamoja na Nicole Lewis-Lettington ambaye ni Mratibu wa Miradi wa  UNCTAD na Paul Akiwumi ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika katika UNCTAD miongoni mwa wengine.

Martin Mwanje & PCS
+ posts

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here