Home Habari Kuu Rais Ruto akutana na Jaji Mkuu Martha Koome Ikulu ya Nairobi

Rais Ruto akutana na Jaji Mkuu Martha Koome Ikulu ya Nairobi

0

Rais William Ruto leo Jumatatu anakutana na Jaji Mkuu Martha Koome katika Ikulu ya Nairobi. 

Hii ni kwa mujibu wa msemaji wa mawasiliano ya umma wa Ikulu ya Nairobi Gerald Bitok.

Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu na Maspika Moses Wetang’ula wa bunge la kitaifa na Amason Kingi wa bunge la seneti ni miongoni mwa viongozi wanaosemekana kuhudhuria mkutano huo.

Mkutano huo unakuja siku chache baada ya Rais Ruto kuilimbikizia idara ya mahakama lundo la lawama kwa kushirikiana na watu fulani kuhujumu miradi ya serikali.

Ni Shutuma zilizomfanya Jaji Koome kutaka kushiriki mkutano na Rais Ruto ili kuangazia masuala ibuka.

Upinzani ukiongozwa na Raila Odinga sawia na chama cha wanasheria nchini, LSK walipinga kufanyika kwa mkutano kati ya Rais Ruto na Jaji Koome wakihofia kuwa utahujumu utendakazi wa serikali, pingamizi ambazo sasa zimeambulia patupu.

 

Website | + posts