Home Habari Kuu Rais Ruto akaa ngumu kwa madaktari wanaogoma

Rais Ruto akaa ngumu kwa madaktari wanaogoma

0

Mgomo wa madaktari ambao unakaribia miezi miwili tangu uanze huenda ukadumu kwa muda mrefu zaidi ilivyotarajiwa, baada ya serikali kukiri kukosa pesa za kuwalipa.

Akihutubu siku ya Jumatano katika sherehe za Leba Dei, Rais William Ruto alijitokeza kimasomaso na kusema kuwa serikali imekubaliana na madaktari kwa matakwa  17 kati ya 19, ila kwa mawili yaliyosalia hawana uwezo wa kutekeleza kwani serikali haina pesa.

Badala yake, Ruto aliwataka madaktari kurejea kazini.

Matamshi haya yanajiri huku makundi mbalimbali ya wafanyakazi yakiapa kujiunga na mgomo huo kama njia ya kuishinikiza serikali kuwapa nyongeza ya mishahara.

Huduma za afya katika hospitali zote za umma nchini  zimelemazwa tangu kuanza kwa mgomo huo, huku walio na hela pekee wakitibiwa katika hospitali za kibinafsi.

Website | + posts