Home Habari Kuu Rais Ruto aidhinisha kuondoka kwa kundi la kwanza la polisi 400 kwenda...

Rais Ruto aidhinisha kuondoka kwa kundi la kwanza la polisi 400 kwenda Haiti

0
kra

Rais William Ruto amekabidhi bendera ya taifa kwa kundi la kwanza la polisi 400 wanaoelekea nchini Haiti kudumisha utulivu na usalama.

Polisi hao watakaosafiri kati ya leo na kesho Jumanne ni sehemu ya maafisa 1,000 anbao serikali ya Kenya iliahidi kutuma nchini Haiti ili kukabiliana na magenge yanayowahangaisha raia nchini Haiti.

kra

Polisi hao wanajumuisha wale wa Rapid Deployment Unit (RDU), Anti Stock Theft Unit (ASTU), General Service Unit (GSU), na Border Patrol Unit (BPU).

Maafisa hao tayari wamepokea mafunzo katika sekta mbalimbali kama vile lugha.

Kiongozi wa operesheni hiyo aliyeteuliwa atauwa Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi Godfrey Otunge huku Kenya ikilenga kutuma takriban maafisa 2,500.

Serikali ya Marekani itagharimia mishahara ya polisi hao pamoja na gharama zote zinazohusiana na operesheni hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here