Home Taifa Rais Ruto ahimiza umoja na ushirikiano kati ya Wakenya

Rais Ruto ahimiza umoja na ushirikiano kati ya Wakenya

0
kra

Rais William Ruto amehimiza Wakenya wote wawe na umoja na washirikiane ili kuhakikisha ufanisi wa taifa hili.

Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Petero, Ngambwa, kaunti ya Taita Taveta eneo la Pwani, kiongozi wa nchi alisema wakati umewadia wa viongozi wote kuweka kando tofauti za kisiasa na kushirikiana katika kuimarisha Kenya.

kra

Alielezea nia yake ya kushirikiana na viongozi wote na vyama vyote vya kisiasa kuanzia sasa.

Kando na hilo Rais alihimiza vijana kutumia vituo vya kidijitali ambavyo serikali imeweka na inaendelea kuweka katika sehemu mbali mbali nchini kujiatia riziki.

Baadaye jana jioni kiongozi wa nchi alifanya mkutano na wananchi jijini Mombasa ambapo alikabiliwa na masuali.

Rais William Ruto amekuwa akifanya ziara ya kimaendeleo katika eneo la Pwani ambapo amezuru na kuzindua miradi kadhaa ya kimaendeleo.

Ziara hiyo ilijiri baada yake kutoa orodha ya pili ya mawaziri wateule ambapo amemteua Ali Hassan Joho na Salim Mvurya na wadadisi wanachukulia ziara yake kuwa iliyolenga kupoza joto la maandamano nchini.