Home Habari Kuu Rais Ruto ahimiza kuimarishwa ushirikiano kati ya Saudia na Afrika

Rais Ruto ahimiza kuimarishwa ushirikiano kati ya Saudia na Afrika

Rais pia aliyataka mataifa ya kiarabu,  kukumbatia nafasi za kibiashara zilizopo barani afrika kupitia, mkataba wa biashara huru wa bara Afrika (AfCFTA).

0

Rais William Ruto ametoa wito wa kuboreshwa ushirikiano baina ya Saudi Arabia na bara la Afrika, katika ustawishaji wa raslimali ya kawi safi.

Rais alielezea umuhimu wa ushirikiano dhabiti kushughulikia mahitaji ya sasa na siku za usoni ya nishati kwa kuzingatia changamoto zilizopo kuhusu nishati ulimwenguni.

“Ushirikiano kati ya Saudi Arabia na Afrika katika ustawishaji wa kawi safi, unatoa fursa ya kuafikia mahitaji ya sasa na ya siku zijazo ya kawi na pia kutatua changamoto zinazoshuhudiwa kote duniani,” alisema Rais Ruto.

Rais pia aliyataka mataifa ya kiarabu,  kukumbatia nafasi za kibiashara zilizopo barani afrika kupitia, mkataba wa biashara huru wa bara Afrika (AfCFTA) unaofanya Kenya kuwa kitovu cha biashara kwa mataifa mengi barani.

Aidha kiongozi wa taifa alihoji umuhimu wa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya milki za kiharabu na Afrika kama nguzo muhimu katika ukuzaji udhabiti wa kanda na ulimwengu kwa ujumla.

Rais aliyasema hayo alipohutubia kongamano la tano baina ya Saudi Arabia na Afrika jijini Riyadh, Saudi Arabia.

Viongozi waliohudhuria kongamano hilo ni pamoja na mfalme wa Saudia Salman bin Abdulaziz al Saud,  Waziri mkuu wa Saudi Arabia, Rais wa Comoros ambaye pia ni mwenyekiti wa muungano wa Afrika  Azali Assoumani, Katibu mkuu wa muungano wa Milki za kiarabu Ahmed Aboul Gheit na mwenyekiti wa muungano wa tume ya Afrika Moussa Faki miongoni mwa wengine.

Website | + posts