Rais William Ruto, amefungua mradi wa unyunyuziaji wa Bura katika eneo la Bura,kaunti ya Tana River unaolenga kuongeza uzalishaji chakula nchini.
Mradi huo unatarajiwa kupanuliwa kutoka eneo la ardhi la ekari 12,000 hadi ekari 25,000.
Mradi huo unalenga kuongeza uzalishaji wa mpunga kufikia magunia 950,00 na magunia nusu milioni ya mahindi kila mwaka.
Rais Ruto amesema kuwa upanuzi wa eneo la ardhi la mradi huo litaongeza nafasi za ajira mpya 120,000 na kuinua uchumi wa Kenya kwa shilingi bilioni 5 kwa kila mwaka.
Ruto aliandamana na naibu wake Rigathin Gachagua kwenye ziara ya Jumamosi eneo la Bura Tana ambapo baadaye walikagua ujenzi wa barabara ya kilomita 26 .